Bøger i Mnadhifishaji serien i rækkefølge

Filter
Filter
Sorter efterSorter Serie rækkefølge
  • af Inger Gammelgaard Madsen
    Fra 9,95 kr.

    Bertram na marafiki wake watatu; Jack, Kasper na Felix, wamekamilisha masomo yao hivi punde na kutengeneza genge ndogo la muda na kujiita The Hawks. Wao wanamfanyia kazi The Handler, ambaye huwalipa baada ya wao kuvunja maduka na kuuba fanicha bainifu za bei ghali pindi The Handler anapopata agizo kutoka kwa wateja wake. Bertram anaishi yeye na mama yake pekee anayefanya kazi kama mhudumu katika mkahawa. Mamake Bertram anaamini kuwa Bertram anapata pesa zake kutokana na kuwasilisha magazeti. Bertram hawezi kukumbuka mambo mengi kuhusu baba yake. Alikuwa na miaka saba tu wakati baba yake alishikwa baada ya kutekeleza mauaji na kuhukumiwa kifungo cha maisha kwenye jela. Siku moja Bertram anaiba jaketi ya bei ghali iliyotengenezwa kwa ngozi kwenye mkahawa ambao mama yake anafanya kazi. Anapata kitu kilichofichwa katika mfuko ulijificha chini ya bitana ya jaketi ile. Hili linaishia kutokea kwa maafa na sio kwa Bertram tu.The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • af Inger Gammelgaard Madsen
    Fra 9,95 kr.

    Roland Benito, ambaye anakifanyia kazi Kitengo Huru cha Malalamiko kuhusu Polisi, ametumwa pamoja na mfanya kazi mwenza kwenda kuwahoji maafisa wawili wa polisi ambao wameitika mwito wa hali ya dharura. Mlinzi mmoja wa jela amejirusha kutoka kwa dirisha ya chumba chake kilicho katika orofa ya nne, punde tu maafisa hawa wawili wanapowasili baada ya kupata malalamishi kuhusu muziki wa sauti ya juu kutoka kwa chumba hicho. Kwa mtazamo wa juu, hakuonekani kuwa na jambo lolote la kukisiwa kuhusu hali hii ila pale inapotambulika kuwa mlinzi huyu wa jela ni baba ya rafiki wa dhati wa mjukuu wake Roland wanaosoma pamoja, Roland anasikia kuwa mfungwa mmoja amefariki kwenye jela pale alipokuwa akifanya kazi na kuwa mlinzi huyu wa jela amekuwa akihisi kutishiwa na anayefuatwa. Je, inawezekana kuwa haya hayakuwa mauaji ya binafsi hatimaye? Anne Larsen, mwandishi wa habari kutoka TV2 East Jutland, pia ananukuu hadithi ya vifo hivi. Wakati wa utafiti wake, anatambua kifo kingine, wakili wa utetezi aliyefariki katika ajali ya barabarani. Anatambua kuwa vifo hivi vyote vinahusishwa na mfungwa mmoja, Patrick Asp muuaji wa mtoto, ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumuua mtoto wake mdogo wa kike, na ambaye ni mfungwa katika jela ambayo mlinzi yule wa jela alikuwa akifanya kazi.The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • af Inger Gammelgaard Madsen
    Fra 9,95 kr.

    Bertram anaogopa kuenda kwa polisi kuwaambia kuhusu kile alichokipata kwenye jaketi aliyoiba kwani yeye ni mhalifu anayesakwa na hataki jambo lolote linalihusiana na utekelezaji wa sheria. Jioni moja anajaribu kupiga simu bila kujitambulisha huku akiwa amelewa na baada ya kuvuta sigara kadhaa, ila polisi wanakataa kumuamini. Baadaye wakati Bertram anagundua kuwa maisha ya mama yake yamo hatarini, anajaribu kumuonya ila pia mama yake hamuamini. Bertram anaanza kumfuata mama yake na kutambua kuwa anakutana na mwanamume ambaye Bertram hamfahamu. Wakati Bertram anamuuliza mwanamume yule ni nani, mama yake hatimaye anakubali kuwa yule ni mpenzi wake na kuwa wanapanga kuondoka katika eneo lile na kuanza maisha mapya pamoja. Bertram anaamua kupekua ili kujua anapoishi mwanamume huyu, na kuvunja nyumba na kuingia ili kugundua yale atakayoweza kuhusu mwanamume huyu. Anapoangalia vitu vya mwanamume huyu, anapata mkusanyiko wa pasipoti ghushi, na picha ya mwanamume yule akiwa amevalia jaketi ile ambayo Bertram alikuwa ameiba.The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. Baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

  • af Inger Gammelgaard Madsen
    Fra 9,95 kr.

    Habari mpya katika kesi hii inamfanya Roland kuangalia tena mauaji ya mlinzi yule wa jela. Kwa sasa ana uhakika kuwa anamfahamu Uwe Finch na anaamua kumfahamisha Anne Larsen. Anne ndiye alipata michoro ya vidole vya Uwe Finch, na kwa muda uliopita, Roland ametambua kuwa Anne anaweza kuwa mtu wa msaada mkubwa katika uchunguzi wa polisi. Bertram anashtuka kutambua kilichomfanyikia mama yake ila kwa mara moja Anne Larsen, mwanahabari kutoka TV2 East Jutland, anafika. Bertram anaangua kilio mbele ya Anne huku akimueleza mambo yote na Anne anamuambia kuwa wanahitaji kuondoka mara moja. Ila muda umeyoyoma. Wakati Roland anasikia kuhusu kifo kipya kupitia redio ya gari lake anahofia kuwa huenda Anne Larsen ako hatarini pia na anajaribu kumpigia simu ila hapati majibu. Anapopokea simu, anatumai kuwa ni Anne ila inageuka na kuwa ni Leif Skovby, ofisa mmoja katika kesi ile ya mauaji. Leif anataka kuonana naye Roland, na kile anachomwambia kinafanya mambo yote kubainika. Roland anamtumia ofisa huyu kumsaidia kupata simu ya Anne ila, je, Roland atampata Anne kabla ya muda kuyoyoma?The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. Baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).